Mafunzo ya ujasiriamali kwa akina mama mkoani Morogoro

Mafunzo ya ujasiriamali kwa akina mama mkoani Morogoro
Mafunzo ya ujasiriamali kwa akina mama mkoani Morogoro

YSMF inaendesha mafunzo ya ujasiriamali kwa akina mama wenye umri mdogo ,Sisi kama YSMF tunaamini katika falsafa ya kuinuka baada ya kujikwaa na kwamba ipo nguvu kubwa kwa anayeinuka baada ya kujikwaa,ipo dira kubwa inajiinua,ipo ndoto kubwa inayojitokeza tena kwa mara nyingine ya kuitimiza, Hivyo YSMF tumekuwa mstari wa mbele kuwasaidia wanawake au watoto wa kike ambao katika umri wao mdogo wamejikuta wakipata ujauzito na kujifungua mtoto/watoto. Hali hii katika jamii zetu za kitanzania imekuwa haina mapokeo mazuri,wamama hawa wadogo wadogo wamekuwa....

 • Wakitengwa katika jamii
 • Wakikatisha masomo
 • Wakitishiwa maisha
 • Wakijichukia na kujiona wakosaji
 • Wakati mwingine kufanyiwa ukatili mkubwa.

Sisi kama YSMF tuko mstari wa mbele katika kuhakikisha huyu mtoto wa kike mzazi anapata...

 • Anapata nafasi nyingine
 • Anapata fursa nyingine
 • Anapata dira nyingine
 • Anapata mwanga mpya
 • Na zaidi ya yote kufufua ndoto zake upya.

YSMF tunateleza miradi kadhaa ya kumlenga mtoto huyu wa kike ambaye amekuwa mzazi katika umri mdogo.Pamoja na mengine YSMF tunaendesha mafunzo yaliyoanza tarehe 12/09/2016 mpaka 07/10/2016 mjini Morogoro kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.Mafunzo haya yanahusu ujasiriamali na mikopo kwa akina mama,yenye malengo ya kuwainua kiuchumi wazazi hawa wenye umri mdogo.Mafunzo haya pia yanatajielekeza katika uundwaji wa vikundi vya akina mama kwaajili kijikwamua kiuchumi na namna ya kubuni na kusimamia miradi midogo midogo,ufuatiliaji wa matokeo chanya ya Mafunzo kwa washiriki ikiwa na pamoja na kutoa vyeti kwa washiriki wote,kwa wastanii kuna washiriki zaidi ya 50 kutoka mkoani Morogoro.

YSMF tunaamini katika kuanza upya,hivyo kama taasisi kwa mchango wetu mdogo tunawaanda wamama wenye umri mdogo katika kuamini kuwa wanaweza,tunawahamisha,tunavuka nao na kuambatana nao katika nyakati ngumu,mpaka kufikia mwangaza,faraja na kwenye neema.

YSMF"The home of hope and inspiration "

 • Google+
 • PrintFriendly